Matumizi Mabaya ya Madaraka au Ofisi 🏛️
Kwa mujibu wa Kifungu cha 96 cha Kanuni ya Adhabu, mtu yeyote anayefanya kazi katika utumishi wa umma na anayetumia madaraka yake vibaya kwa kufanya au kuagiza kufanyika kwa kitendo cha kiholela kinachodhuru haki za mtu mwingine, anatenda kosa la jinai.
🔹 Iwapo kitendo hicho kilifanyika kwa nia ya kupata faida, mtumishi huyo akithibitika na kuhukumiwa, anaweza kufungwa hadi miaka mitatu.
🔹 Hata hivyo, mashtaka kwa kosa hili hayawezi kuanzishwa bila idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
⚖️ Hii inalenga kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka ya umma yanayoweza kuathiri haki za watu na kuharibu imani kwa taasisi za serikali.
#MatumiziMabayaYaMadaraka #SheriaZaTanzania #HakiKwaWote #JunguLaSheria ⚖️

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿