🟢 JE, UNAJUA?
Kwa mujibu wa Kifungu cha 186(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai [Sura ya 20, R.E. 2022], mahakama zote zinapaswa kuwa wazi kwa umma! ⚖️👨🏾⚖️
📍 Sheria inasema kuwa eneo lolote ambalo mahakama inatumika kwa ajili ya kusikiliza au kuamua kosa la jinai "litahesabiwa kuwa ni mahakama ya wazi ambayo umma kwa ujumla wanaweza kuhudhuria kadiri nafasi inavyoruhusu."
🔒 Hata hivyo, Jaji au Hakimu anaweza kuamuru baadhi ya vikao kufanyika kwa faragha ikiwa ni kwa maslahi ya haki, usalama wa taifa, maadili ya umma, au ulinzi wa watoto na faragha ya wahusika.
👉 Hii ni haki yako kama raia — kuhudhuria vikao vya wazi vya mahakama ili kushuhudia namna haki inavyotendeka. Ni njia mojawapo ya kuimarisha uwazi, uwajibikaji na kuondoa woga katika mfumo wa utoaji haki.
#MahakamaNiYaUmma#Uwajibikaji #SheriaKwaWote #HakiZaBinadamu #JunguLaSheria #Tanzania.
%20cha%20Sheria%20ya%20Mwenendo%20wa%20Mash_20250417_175024_0000.png)
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿