Kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Ndoa.
Mwanaume aliye katika ndoa ya mke mmoja haruhusiwi kufunga ndoa nyingine. Pia, mwanaume aliye katika ndoa ya wake wengi haruhusiwi kufunga ndoa ya mke mmoja. Mwanamke aliye kwenye ndoa yoyote haruhusiwi kuolewa tena wakati ndoa yake bado ipo. Hata hivyo, wanandoa wanaweza kurudia sherehe ya ndoa, lakini haitabadilisha hali halali ya ndoa yao ya awali.
#JunguLaSheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿