Kwa mujibu wa Kifungu cha 59 cha Sheria ya Ndoa, mume au mke hawezi kuuza au kugawa nyumba ya ndoa, inayomilikiwa kwa pamoja bila ridhaa ya mwenzi wake. Mwenza huyo anayo haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo hata kama haijasajiliwa kwa jina lake hadi ndoa itakapovunjwa au mahakama iamue vinginevyo. Pia, mwenza aliyeachwa hawezi kufukuzwa katika nyumba ya ndoa bila maagizo ya mahakama.
#HakiZaWanandoa #NyumbaYaNdoa #SheriaYaNdoa #JunguLaSheria 🇹🇿

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿