Ticker

6/recent/ticker-posts

💔 Haki ya Kudai Fidia Baada ya Ahadi ya Ndoa kuvunjika!💍⚖️



💔 Haki ya Kudai Fidia Baada ya Ahadi ya Ndoa kuvunjika!💍⚖️

Kwa mujibu wa Kifungu cha 69 cha sheria ya ndoa, mtu ana haki ya kudai fidia ikiwa mchumba wake amevunja ahadi ya ndoa na kupelekea hasara ya fedha au mali. Hata hivyo, fidia haiwezi kudaiwa endapo ahadi ya ndoa ilitolewa wakati mdaiwa akiwa na umri chini ya miaka 18. Na fidia itatolewa kulingana na kiasi cha hasara iliyopatikana tu na si zaidi ya hapo.

💡 Aidha, hakuna shauri linaloruhusiwa kisheria kufunguliwa kulazimisha kutimizwa kwa ahadi ya ndoa ambayo haijatimizwa.

Shauri la kudai fidia linaweza kufunguliwa hata kwa ahadi za ndoa zilizotolewa nje ya Tanzania lakini kwa kigezo tu kwamba, sheria za nchi hiyo na Tanzania zinakubali.

#AhadiYaNdoa #HakiZangu #Fidia #SheriaTanzania #JunguLaSheria

Chapisha Maoni

0 Maoni