📜 Kwa mujibu wa Kifungu cha 72 cha Sheria ya Ndoa
💍 Mume au mke ana haki ya kufungua shauri la madai ya fidia 🏛️ dhidi ya mtu yeyote aliyefanya uzinzi na mwenzi wake wa ndoa.
⚖️ Hata hivyo:
🔹 Shauri haliwezi kukubalika iwapo mlalamikaji aliridhia tendo hilo.
🔹 Shauri haliwezi kufunguliwa iwapo fidia tayari imedaiwa kupitia shauri la talaka 💔.
🔹 Shauri litafutwa ikiwa mtuhumiwa atathibitisha kuwa hakujua kuwa mtu aliyefanya nae uzinzi alikuwa ameoa/kuolewa 🙅🏽.
✍🏽 #SheriaYaNdoa #JungulaSheriaTanzania

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿