Ticker

6/recent/ticker-posts

Mfanyakazi ana haki ya likizo ya mwaka ya siku 28 mfululizo katika kila mzunguko wa mwaka.

 


📌 Kwa mujibu wa Kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini; ⚖️

👩‍⚕️ Mfanyakazi ana haki ya likizo ya mwaka ya siku 28 mfululizo katika kila mzunguko wa mwaka. Siku hizi za likizo zinajumuisha pia sikukuu za kitaifa zitakazoangukia ndani ya kipindi cha likizo.

Iwapo mfanyakazi, kwa ombi lake, alipewa likizo ya muda ndani ya mwaka, siku hizo zinaweza kupunguza idadi ya siku za likizo ya mwaka. 📜

👨‍💼Mwajiri ana mamlaka ya kuamua lini likizo itatumika, lakini lazima itumike ndani ya miezi sita baada ya mwaka wa likizo kuisha, au ndani ya miezi kumi na miwili endapo mfanyakazi ameridhia na kuna sababu za kiutendaji kazini.

Aidha, mwajiri anatakiwa kumlipa mfanyakazi mshahara wake wote kabla ya kuanza likizo. Kwa ridhaa ya mfanyakazi, anaweza kuitwa kufanya kazi wakati wa likizo ya mwaka, lakini haruhusiwi kufanya kazi mfululizo kwa kipindi cha miaka miwili bila kutumia likizo ya mwaka.

#ajira #kazi #sheriayakazi #mwajiri #mwajiriwa

Chapisha Maoni

0 Maoni