DHANA YA KUCHUKULIA NDOA:
Kuna dhana inayokanushika (rebuttable presumption) kuwa mwanaume na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa.
Ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.
(i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamume wameishi pamoja kwa muda wa miaka 2 au zaidi kwa mfululizo.
(ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma unaowazunguka unawachukulia na kuwapa heshima kama mke na mume.
(iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume wakati walipoanza kuishi pamoja kama umri ulikubalika kisheria.
(iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa inayoendelea.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿