Ticker

6/recent/ticker-posts

Je, umewahi kuitwa kazini siku ya sikukuu ya kitaifa au umma.



JE UMEWAHI KUITWA KAZINI SIKU YA SIKUKUU YA KITAIFA AU UMMA?

Kwa kawaida katika nchi yetu kuna sikukuu za umma kama zinavyotambuliwa na sheria ya sikukuu za umma. Kwa kawaida siku hizi ni za mapumziko kwa watu wote lakini baadhi ya wafanyakazi wanaweza kuitwa kuendelea na kazi katika siku hizi za sikukuu za umma kwa malipo maalumu.

Endapo utaitwa kufanya kazi katika sikukuu hizi za umma, unapaswa kulipwa nyongeza ya mshahara kutokana na masaa ya ziada uliyofanya kazi. 

KIFUNGU namba 25 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini kinasema " Kama mfanyakazi atafanya kazi wakati wa sikukuu zilizotajwa katika Sheria ya Sikukuu za Umma, mwajiri atatakiwa kumlipa mfanyakazi mara mbili ya ujira wa kawaida kwa kila saa atakayofanya kazi siku hiyo.

Tupigie tuongee kwa suala lolote linalokutatanisha.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni