Je unaijua tafsiri ya kusababisha kifo katika sheria?
Kusababisha kifo kama inavyoelezwa katika KANUNI YA ADHABU sura ya 16, ni kukatisha maisha ya mtu kwa njia yoyote ile ndani ya siku ya tukio au ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu tukio kutokea endapo sababu za kifo zitakuwa ni zile zilizotokana na kitendo alichofanyiwa marehemu.
MFANO. Ukimshambulia mtu na kumdhuru au kuumiza mwili wake, hata asipofariki siku ya tukio, lakini akafariki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kutokana na sababu za kushambuliwa, basi mshambuliaji atakabiliwa na mashtaka ya mauaji.
Endelea kujifunza kwa kuwa nasi, KARIBU.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿