Ticker

6/recent/ticker-posts

Je, umewahi kupigwa na polisi bila sababu yoyote ya msingi.


JE UMEWAHI KUPIGWA NA POLISI BILA SABABU YOYOTE YA MSINGI?

Kwa sheria tulizonazo sasa, ni kosa kisheria na ni kosa kimaadili kwa polisi kumpiga raia, mtuhumiwa au mtu yeyote bila sababu iliyohalalishwa kisheria.

Endapo wewe ni mtuhumiwa wa uhalifu fulani na upo mikononi mwa polisi unatakiwa kutii amri halali na ambazo hazizalilishi na kutweza utu wa mtu kwani mtuhumiwa si lazima awe mtenda kosa ni tuhuma mpaka zithibitishwe mahakamani.

Polisi anaruhusiwa kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa atakapo jaribu kukimbia, kukataa kukamatwa, au endapo mtuhumiwa atajaribu au kushambulia askari.

Endapo umepigwa na polisi na kukusababishia madhara unaweza kuripoti uhalifu huo kwa mkuu wa kituo cha mahali ulipopatwa na kadhia hiyo na ukiona haki haifanyiki wepesi unaweza kufungua kesi ya madai mahakamani.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni