JE UNAJUA UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA MGOGORO WA ARDHI?
Kama una mgogoro wa ardhi na umejaribu kuumaliza kwa njia ya mazungumzo na imeshindikana unaweza kufuata utaratibu ufuatao;
1. Nenda baraza la ardhi la kijiji anzisha shauri lako (hasa kwa ardhi zilizopo vijijini na ambazo hazijasajiliwa wala kupimwa)
2. Baraza la usuluhishi la nyumba(makazi) na ardhi la kata (endapo suluhu ikikosekana katika baraza la ardhi la kijiji unaenda katika baraza la kata)
3. Baraza la usuluhishi la nyumba(makazi) na ardhi la wilaya (endapo suluhu ikikosekana katika baraza la ardhi la kata unaenda katika baraza la wilaya)
4. Mahakama kuu kitengo cha ardhi (endapo suluhu ikikosekana katika baraza la ardhi la wilaya unaenda mahakama kuu kitengo cha ardhi ndani ya siku sitini baada ya hukumu kutolewa na baraza la nyumba na ardhi la wilaya)
Mawasiliano yetu yako wazi, karibu kwa maongezi.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿