Ticker

6/recent/ticker-posts

Sheria ndogo.


UMEWAHI KUSIKIA KITU KINAITWA SHERIA NDOGO?

Kwa kawaida jukumu la kutunga sheria lipo mikononi mwa bunge lakini kutokana na ufinyu wa muda wa bunge na masuala ya kiufundi kuna sheria zingine ambazo hutungwa na idara au taasisi za serikali nje ya bunge kwa kibali cha bunge, sheria hizo huitwa SHERIA NDOGO.

Kamwe sheria ndogo haitakiwi kukinzana na sheria mama ya bunge au kuifanya sheria mama kukosa maana. sheria ndogo huweza kuitwa orders, subsidiary legislation, by laws na majina mengine kadha wa kadha.

Sheria mama au parent law kwa kawaida hutungwa na bunge pekee na ndio sheria ambayo hutumika mahakamani pamoja na miongozo yake.

Sheria ndogo ndogo hutumika mara nyingi katika maeneo madogo madogo Kama vile wilaya, kata, tarafa, mtaa au mkoa. Mara nyingi Sheria ndogo huwa hazitumiki kufanya kazi nchi nzima.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni