Ticker

6/recent/ticker-posts

Ufafanuzi wa sheria kuhusu ubakaji. Na Johnson Yesaya


Ufafanuzi wa kubaka katika sheria ya kanuni ya adhabu au penal code kifungu cha 130, 131 na 132

130. Mtu yeyote ambaye bila halali atamuundama mwanamke au msichana bila idhini yake, au kwa idhini yake ikiwa idhini kaipata kwa nguvu au kwa njia ya kuhofisha au kutishia kwa namna yoyote au kwa hofu ya kuumizwa kiwiliwili, au kwa njia ya madanganyo juu ya namna ya kitendo chenyewe kilivyo au, kwa upande wa muolewa, kwa kujifanya ni mumewe, mtu huyo amekosa kosa kubwa liitwalo “kubaka”.

Adhabu ya kubaka

131. Mtu yeyote ambaye atatenda kosa la kubaka atapasiwa adhabu ya kifungo cha maisha pamoja na kutandikwa au bila kutandikwa.

Jaribio la kubaka

132. Mtu yeyote ambaye atajaribu kubaka amekosa kosa kubwa na atapasiwa kifungo cha maisha pamoja na kutandikwa au bila ya kutandikwa.

Lakini pia endapo mtenda kosa hatafungwa maisha, basi kifungo kisipungue miaka thelathini.

Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni