Kutakatisha fedha ni njia au mbinu zozote zinazotumika kugeuza fedha haramu ambazo zimepatikana kinyume cha sheria (wizi, rushwa, ukwepaji kodi n.k) na fedha hizo huingizwa kwenye mifumo halali ya kifedha kama mabenki au kwa kuwekezwa katika biashara halali ili ziweze kutumika kama fedha halali.
Utakatishaji fedha unaweza kufanywa kwa kujua au kwa kutokujua kupitia benki, fedha za mtandaoni na katika biashara ya kubadili fedha za kigeni (foreign exchange).
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿