Kifungu cha ishirini na moja (section 21) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (Criminal procedure Act Cap 20)
Kinamtaka polisi kutotumia nguvu za kupita kiasi katika zoezi na ukamataji wa watuhumiwa wa makosa ya jinai. Pia kifungu hicho kinamkataza polisi kufanya kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisa kifo kwa mkamatwaji.
Lakini polisi anaruhusiwa kusababisha kifo endapo mkamatwaji atakuwa katika hali ya kusababisha vifo kwa watu wengine au kutaka kuwashambulia polisi kwa silaha za moto.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿