MAHAKAMA ZIPI ZINA MAMLAKA YA KUSIKILIZA MASHAURI YA MIRATHI.
Mirathi inaweza kufunguliwa katika mahakama mbalimbali kutegemea na sheria itakayosimamia mirathi husika.
A) Kama sheria ya kimila itatumika katika kugawa mirathi basi shauri la kuomba usimamizi wa mirathi litafunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo. Msimamizi wa mirathi anatakiwa airidhishe mahakama kwamba marehemu kutokana na maneno yake, mfumo wake wa maisha au maandishi aliyoacha, alionyesha nia kwamba mirathi yake alitaka iendeshwe kwa kufuata sheria za kimila.
B) Kama sheria itakayotumika ni ya kiisilamu basi shauri la kuomba usimamizi wa mirathi litafunguliwa Mahakama ya Mwanzo. Msimamizi wa mirathi anatakiwa airidhishe mahakama kwamba marehemu kutokana na maneno yake, mfumo wake wa maisha au maandishi aliyoacha, alionyesha nia kwamba mirathi yake alitaka iendeshwe kwa kufuata sheria za kiislamu.
C) Kama sheria itakayotumika kugawa mirathi ni ya Serikali basi mahakama wilaya, mahakama ya hakimu mkazi na mahakama kuu zinahusika kutegemea thamani ya mali alizoacha marehemu.
i. Thamani ya mali yote aliyoiacha marehemu isiyoondosheka isiyozidi shilingi milioni 5 (Mfano nyumba, mashamba) na inayoondosheka isiyozidi shilingi milioni 3 (mfano magari) mirathi ya aina hii inafunguliwa Mahakama ya Mwanzo.
ii. Thamani ya mali yote aliyoiacha marehemu isiyohamishika isiyozidi shilingi milioni 12 na inayohamishika isiyozidi shilingi milioni 100 mirathi hii inafunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ama ya Hakimu Mkazi.
iii. Thamani ya mali inayozidi shs millioni 150 mirathi hii inafunguliwa mahakama Kuu.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿