SHERIA IMETAJA WATU WA AINA GANI AMBAO WANAWEZA KUWA WASIMAMIZI WA MIRATHI?
A] Ndugu wa marehemu na wale wenye maslahi na mirathi ya marehemu, kwa mfano wale ambao wanatarajia kupata sehemu ya mirathi ya marehemu.
B] Mtu au watu wanao mdai marehemu, Mtu huyu hufungua mirathi pale ambapo ndugu wa marehemu wameshindwa au hawataki kufungua mirathi.
C] Msimamizi mkuu wa mirathi, huyu au hii ni ofisi ya serikali ambayo hujihusisha, Pamoja na mambo mengine, usimamizi wa mirathi, endapo itaombwa na mtu yeyote.
D] Muwakilishi wa kisheria, mtu aliyetajwa kama msimamizi wa mirathi [mtu aliyepewa power of attorney]
E] Mtu yeyote ambaye mahakama kwa kuangalia vigezo mbalimbali vikiwamo udugu, maslahi ya muhusika katika mirathi hiyo, usalama wa mali za mirathi pamoja na uwezekano wa kuisimamia vizuri, anaweza kuteuliwa na mahakama
VILEVILE Sheria imetoa baadhi ya vigezo ambavyo mtu lazima awe navyo ili apate usimamizi wa mirathi.
I]awe mtu mzima
II]awe na akili timamu
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿