UTARATIBU UTUMIKAO KATIKA KUOMBA USIMAMIZI WA MIRATHI MAHAKAMANI
A. KAMA KUNA WOSIA WA MAREHEMU
1. Taarifa ya kifo iandikishwe kwa mkuu wa wilaya ndani ya siku 30
2. Msimamizi wa mirathi aende akafungue mirathi mahakamani akiwa na;
a]wosia uliachwa na marehemu
b]Cheti cha kuthibitisha kifo cha marehemu
3. Mahakama hutoa tangazo la maombi ya kuteuliwa msimamizi wa mirathi kwa muda wa siku 90, lengo la tangazo ni kwamba kama mtu yeyote anapingamizi dhidi ya wosia au msimamizi wa mirathi basi awasilishe mahakamani. Kama hakuna tatizo lolote msimamizi hukabidhiwa barua ya kuhalalisha uteuzi wake na majukumu yake
B.KAMA HAKUNA WOSIA WA MAREHEMU
1. Kifo kiandikishwe kwa mkuu wa wilaya ndani ya siku 30
2. Mkutano wa ukoo ufanyike kuchagua msimamizi wa mirathi
3. Msimamizi wa mirathi aende kufungua mirathi mahakamani akiwa na nakala ya uamuzi wa ukoo na cheti cha kifo
4. Tangazo hutolewa na mahakama kwa muda wa siku 90. Kama hakuna matatizo, msimamizi hukabidhiwa barua ya kuhalalisha usimamizi wake.
Jungu Attorneys at Jungu La Sheria Tanzania.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿