Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugaidi ni nini? Na Johnson Yesaya. LL.B.



 UGAIDI NI NINI?

Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii ya kimataifa na vyombo vyake.

Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.

Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.

Ugaidi una madhara makubwa kwa watu na vitu na ni tishio kubwa la usalama katika dunia ya sasa. Maelfu ya vifo katika karne hii ya 21 yanatokana na ugaidi, ambapo magaidi wana lenga raia wasio na hatia.

Tanzania ilikubwa na tukio lakigaidi mwaka 1998 lililoacha vifo vya baadhi ya watu. Tukio hili lilielekezwa katika ubalozi wa marekani hapa nchini. Wakati huohuo magaidi walishambulia ubalozi wa marekani jijini Nairobi, Kenya.

Sheria ya kudhibiti ugaidi.

Sheria hii imejinaisha ugaidi, katika ngazi tofauti. Kuanzia kutenda au kujihusisha na vitendo vya kigaidi, ikiwemo kusaidia magaidi, kushauri, kudhamini fedha au vitu vitakavyopelekea ugaidi kutendeka.

Nguvu ya kutangaza mtu, jumuiya au kikundi cha watu kua cha kigaidi.

Sheria imempa mamlaka waziri wa mambo ya ndani kumtangaza mtu au kikundi au jumuiya yoyote kuwa ya kigaidi baada yakujiridhisha kua mtu huyo au kikundi hicho kinajihusisha na ugaidi au mambo yanayoweza kutafsiriwa kua ni ya kigaidi kulingana na vifungu vya sheria. Kifungu No. 12.

Nguvu ya kukamata bila kibali cha mahakama.

Kifungu No. 28 cha sheria hii kimetoa mamlaka kwa afisa polisi, au uhamiaji kukamata bila ruhusa/kibali cha mahakama gaidi au mtu atakaemuhisi kua ni gaidi au anashirikiana na magaidi.

Afisa usalama wa taifa.

Hali kadhalika, kifungu hiki (No. 28) kimetoa mamlaka na nguvu kwa afisa usalama wa taifa kukamata mtu ambae ni gaidi au atamuhisi kuwa ni gaidi.

Mamlaka haya ni yakipekee kwakua sheria ya usalama wa taifa hairuhusu maafisa usalama kukamata wahalifu. TISS wana mamlaka pekee yakukusanya taarifa za kiusalama, kuchambua, kutafsiri nakuwasilisha ripoti kwa raisi au waziri mwenye dhamana.

Jukumu la kutoa taarifa za ugaidi/magaidi.

Kifungu No.40 cha sheria hii kinatoa jukumu la lazima kwa raia au mtu yeyote mwenye taarifa zinazohusu mtu au tukio lakigaidi kuzifikisha polisi ama kwa mrakibu msaidizi wa polisi au mkuu wakituo cha polisi. Mtoa taarifa pia amepewa kinga ya kutokufunguliwa mashtaka yoyote juu yataarifa alioitoa akiwa anaamini ni ya kweli.

Adhabu yakutokutoa taarifa kama kifungu hiki kinavyo hitaji ni kifungo kisicho pungua miaka miwili na kisichozidi miaka mitano.

Baadhi ya makosa na adhabu zake.

1. Kutoa au kukusanya fedha kwa lengo la kufanikisha ugaidi. (kifungo miaka 15-20).

2. Kutoa au kukusanya mali, au kumkaribisha mtu atoe mali au kuweka mazingira ya uwepo wa mali au fedha na huduma zifananazo ili kufanikisha. (kifungo miaka 20-25).

3. Kuwapa silaha magaidi. (miaka 20-30)

4. Kushawishi au kusaidia katika kushawishi watu kujiunga na makundi ya kigaidi. (kifungo miaka 15-20).

5. Kutumia mali, au kumiliki mali kwa njia yoyote ambayo inakusudio lakusaidia kutekeleza ugaidi (kifungo miaka 15-20).

6. Kujimilikisha mali za magaidi kwa lengo la kuficha umiliki wa wahusika ili kuwasaidia kutojulikana, au kuhamisha au kwa nyovyote. (kifungo miaka 15-20).

7. Kuishi na gaidi au kumficha gaidi ili asikamatwe na mamlaka husika. (kifungo miaka 18-30).

8. Kua mfuasi wa kundi la kigaidi. (kifungo kisichopungua miaka 8).

9. Kupanga kikao, au kusaidia kwa vyovyote kikao cha magaidi. (miaka 10-15).

10. Kupanga njama, kusaidia, kujaribu, kuficha, kushauri katika utekelezaji wa ugaidi.


By Mfaume H.

Chapisha Maoni

0 Maoni