KUHARIBU AU KUDHARAU NOTI AU SARAFU YA TANZANIA NI KOSA LA JINAI.
Kumekuwa na tabia ya watu mashuhuri duniani kuonekana wakitupa noti au sarafu za fedha katika maji, kuzichoma moto, kuzitumbukiza chooni, kuzichana, na kuzifanyia mzaha. Kwa sheria za nchi zao yawezekana kuwa sio kosa, lakini kwa sheria za Tanzania ni kosa la jinai.
kuharibu noti au sarafu, au kuonesha dharau au dhihaka kwa noti au sarafu za Jamhuri ya Muungano ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu namba 332A cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2019.
Adhabu ya kosa hili inaweza kufikia hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿