SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI, KIFUNGU NO. 181.
Kwa kawaida kesi ya jinai hufunguliwa katika mahakama yenye nguvu kisheria, iliyopo katika eneo ambako kosa husika limetendeka, au eneo ambako madhara ya tendo hilo la kijinai yalipotokea.
Wakati mtu anatuhumiwa kwa kutenda kosa kwa sababu
ya kitu chochote kilichotendeka au kwa matokeo yoyote ambayo yametokea, kosa linaweza kuchunguzwa kwa undani au kusikilizwa, kama kesi itakavyokuwa, na mahakama iliyo ndani ya mipaka yenye mamlaka ambako kitu chochote hicho kimefanyika au matokeo yoyote hayo yametokea.
#ijuesheria
#jinai
#kesizajinai
#sheria
#jungulasheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿