Ticker

6/recent/ticker-posts

UGAIDI. Mwandishi Johnson Yesaya. LL.B




Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii ya kimataifa na vyombo vyake.
Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.

Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.

Baadhi ya mambo yanayoweza kuangukia katika ugaidi ni kama ifuatavyo;

I. Kufanya kitendo au shambulio linaloweza kuleta uharibifu mkubwa kwa nchi au taasisi za kimataifa

II. Kwa kutumia nguvu kuilazimisha serikali kufanya Jambo fulani kwa nguvu bila matakwa ya serikali yenyewe

III. Kutumia silaha au milipuko kwa lenga la kutisha umma wa watanzania.

IV. Kuteka viongozi wakuu wa kiserikali kwa shinikizo fulani

V. Kula njama, kusaidi, kuwezesha magaidi kufanya ugaidi.

VII. Kumiliki vifaa au dhana, namba, michoro au ramani ya eneo lililolindwa na kutumia vifaa hivyo kwa lengo la ugaidi etc

Kosa la ugaidi linafanana sana na kosa la uhaini ambapo kwa pamoja makosa haya adhabu yake ni kifo au kifungo cha miaka kadhaa kutokana na namna ya ushiriki katika uhalifu huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni