Kifungu cha 186(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 kinasema;
Mahakama yoyote inaweza kukaa kusikiliza kosa lolote siku ya jumapili au siku ya mapumziko na hakuna uamuzi, adhabu au amri itakayopitishwa na mahakama nyingine kubatilisha hukumu hiyo kwa sababu ya ukweli kuwa ilitolewa au ilipitishwa jumapili au siku ya mapumziko;
Lakini mahakama inaweza kukaa jumapili au siku ya mapumziko kwa lengo la kuharakisha kesi, kuokoa gharama au usumbufu kwa wahusika wa kesi.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿