Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, SURA YA 20 na marekebisho yake yote mpaka 2019. KIFUNGU CHA 50 na 51.
kifungu cha 50(1)(a), kinaruhusu kumuhoji mtuhumiwa kwa kipindi cha saa nne kuanzia muda alipochukuliwa kuwa chini ya kizuizi kuhusiana na kosa.
Katika kuhesabu kipindi kinachoruhusiwa cha kumuhoji mtu ambaye yuko kizuizini kuhusiana na kosa, kutahesabika kuwa ni sehemu ya kipindi hicho muda wowote ambao afisa polisi anayepeleleza kosa ameacha kumuhoji mtu au anasababisha mtu huyo kufanya kitendo chochote kinachohusiana na upelelezi wa kosa.
Kipindi cha masaa "4" kinaweza kuongezwa kufikia masaa "12", yaani nyongeza ya masaa "8" endapo kwa sababu za msingi inaonekana mahojiano hayajakamilika. Uongezwaji wa muda wa ziada ni lazima uambatane na maombi kwa hakimu, polisi anayefanya upelelezi kuhusu kesi hiyo anapaswa kuomba kwa hakimu muda wa nyongeza wa mahojiano na kama hakimu ataona inafaa, ataruhusu.
MTU ALIYEHOJIWA KWA ZAIDI YA MASAA KUMI NA MBILI BILA SABABU ZA MSINGI ANAWEZA KUFUNGUA KESI KUDAI FIDIA.
Imeandaliwa na : Jungu la sheria Tanzania.
#ijuesheria
#sheria
#jungulasheria
#mwanasheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿