KESI NDOGO NI NINI?
Nadhani umewahi kusikia maneno haya "kesi ndogo". Na unaweza kuwa na maswali ya kujiuliza je kesi ndogo ni nini?, Hutokea wakati gani? na lengo lake huwa Nini?.
KARIBU
KESI NDOGO ni kesi ambayo hujitokeza katikati wakati kesi ya msingi ikiendelea. Kesi ndogo huibuka kutokana na mapingamizi au maombi ya kisheria yanayoweza kujitokeza wakati kesi ya msingi ikiendelea na kuitaka mahakama kutoa muongozo kuhusu mapingamizi au maombi hayo kabla ya kesi ya msingi kuendelea.
LENGO
Lengo kuu la kesi ndogo huwa ni kuweka sawa kesi katika mlolongo au utaratibu wa kisheria kwa lengo la kuhakikisha kila takwa la kisheria linazingatiwa na maamuzi ya kesi ya msingi yatakayotolewa yawe thabiti bila kuathiriwa na makosa ambayo hayakupewa muongozo sahihi wa mahakama wakati mzima wa usikilizaji wa kesi.
Hakuwezi kuwa na kesi ndogo bila kuwepo kesi ya msingi.
#sheria
#ijuesheria
#sherianajamii
#sheriakiganjani
Tupigie. 0758218269 kwa maelezo zaidi.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿