Ticker

6/recent/ticker-posts

Mazingira mbalimbali yanayotengeneza kosa la ubakaji. Na Johnson Yesaya LL.B.



Ni kosa kwa mtu wa jinsia ya kiume kumbaka msichana au mwanamke.

Mtu wa jinsia ya kiume atakuwa ametenda kosa la kubaka kama atakuwa amefanya tendo la ndoa na msichana au mwanamke chini ya mazingira ambayo yanadondokea kwenye maelezo yafuatayo:

(a) ambaye si mke wake, au awe mke wake ambaye ametengana nae bila ridhaa yake wakati wa tendo la ndoa;

(b) kwa ridhaa yake, pale ambapo ridhaa yake imepatikana kwa kutumia nguvu, vitisho, au kwa kumuogopesha au kumtishia kumuua au kumuumiza au akiwa amezuiliwa isivyo halali;

(c) kwa ridhaa yake pale ambapo ridhaa yake imepatikana wakati ambao alikutwa hana akili timamu au akiwa amelewa kwa kushawishiwa na madawa ya kulevya, kitu au vitu ambavyo amepewa na mtu au watu wengine isipokuwa ikithibitika kuwa kulikuwa na ridhaa mwanzoni kati yao wawili;

(d) kwa ridhaa yake pale ambapo mwanamume alijua kuwa yeye si mume wake, na kuwa ridhaa ilitolewa kwa sababu alifanywa kuamini kuwa yeye ni mwanamume mwingine, ambaye yeye mwenyewe, anaamini kuwa ameolewa nae kihalali;

(e) kwa ridhaa au bila ya ridhaa akiwa chini ya umri wa miaka kumi na nane, isipokuwa kama mwanamke ni mke wake ambaye ana umri wa miaka kumi na tano au zaidi na hajatengana na mumewe.

Mtu yeyote- 

(a) akiwa mtu wa mamlaka, kuchukulia kigezo cha nafasi yake ya mamlaka, na anatenda kosa la kubaka kwa msichana au mwanamke wa mahusiano ya kiofisi au kwa kukosea anamzuia na kumbaka msichana au mwanamke;

(b) akiwa kwenye uongozi au kuwa miongoni mwa wafanyakazi wa mahabusu au sehemu nyingine yeyote ya uangalizi, iliyoundwa 

kisheria au kwa taasisi ya wanawake au watoto kwa kuchukulia kigezo cha nafasi yake na kutenda kosa la kubaka msichana yeyote au mwanamke mfanyakazi mwenzie wa magereza, sehemu ya matunzo au taasisi.

(c) akiwa kwenye uongozi au mfanyakazi wa hospitali, kuchukulia kigezo cha nafasi yake na kutenda kosa la kubaka msichana au mwanamke;

(d) akiwa mganga wa kienyeji kuchukulia kigezo cha nafasi yake na anatenda kosa la kubaka msichana au mwanamke ambaye ni mteja wake kwa nia ya kupata uponyaji.

Chapisha Maoni

0 Maoni