Kifungu cha 286 na 287A cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
MTU yoyote anayetenda kosa la unyang'anyi na wakati akitenda kosa hilo amechukuwa silala yoyote ya hatari au yenye kudhuru au chombo, au amefuatana na mtu mmoja mwingine, au iwapo, papo hapo au mara tu kabla au mara tu baada ya unyang’anyi huo, anamjeruhi, anampiga, anamgonga au anatumia nguvu yoyote kwa mtu yeyote, atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha ikiambatana na au bila ya kuambatana na adhabu ya viboko.
Kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha likifanywa bila kujeruhi, kuumiza, kupiga au kuchapa waathirika wa tukio hilo, adhabu yake ni kifungo cha miaka isiyopungua thelalathini kama ilivyoelezwa na kifungu cha 287A Cha kanuni ya adhabu sura ya 16.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿