Ticker

6/recent/ticker-posts

FIDIA KWA KUMSAIDIA POLISI. Na Johnson Yesaya. LL.B



KIFUNGU CHA 37(1), (2) na (3) Cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marekebisho ya 2019.


Pale mtu yeyote anapata hasara  ya mali au maumivu ya mwili, au  anakufa kutokana na kuchukua hatua au katika harakati za kumsaidia hakimu, afisa polisi au  afisa mwingine wa sheria kuzuia utendekaji wa kosa au katika  kumkamata mtu ambaye  ametenda au anadhaniwa kwa  sababu za msingi kuwa  ametenda kosa, atatakiwa kupata  fidia kwa ajili ya hasara au maumivu na kama atakufa, wategemezi wake au wawakilishi  wake kisheria watakuwa na haki  ya kupokea fidia ambayo mtu huyo angepokea kama  asingekufa.


Kiwango cha fidia kitakacholipwa kitakadiriwa, na  mambo mengine yote yahusuyo  malipo ya fidia yatashughulikiwa,  kulingana na masharti ya sheria  iliyopo kwa wakati huo kuhusiana  na malipo ya fidia kwa waathirika  wa makosa ya Jinai.

Chapisha Maoni

0 Maoni