kutupa noti za fedha katika maji, kuzichoma moto, kuzitumbukiza chooni, kuzichana, na kuzifanyia mzaha ni kosa la jinai TANZANIA.
kuharibu noti, au kuonesha dharau au dhihaka kwa noti za fedha za Jamhuri ya Muungano ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu namba 332A cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2019.
KIFUNGU hicho kinasema "Mtu yeyote, bila mamlaka, kwa kunuwia anaharibu, anachana, anakata au vinginevyo anachanachana noti yoyote ya benki au fedha ambayo inatumika kihalali, atakuwa anatenda kosa, na atakuhumiwa kutoa faini ya shilingi "LAKI TANO" kwa kila noti iliyoharibiwa au, akishindwa kulipa faini, atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha mwaka moja.
ADHABU NI FAINI YA LAKI TANO KWA KILA NOTI ILIYOHARIBIKA AU KIFUNGO MWAKA MMOJA.
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿