KIFUNGU CHA 23 CHA SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20 ILIYOREJEWA MWAKA 2019.
Mtu anayemkamata mtu mwingine atalazimika kisheria, wakati wa ukamataji, kumwambia mtu huyo kosa ambalo anakamatwa kwalo.
Mtu anayemkamata mtu mwingine atachukuliwa kuwa ametimiza hayo iwapo atamwambia mtu huyo kiini cha kosa ambalo anakamatwa kwalo; na sio lazima kufanya hivyo katika lugha sahihi kabisa au ya kitaalamu.
Hakutakuwa na ulazima wa kufahamishwa kosa ambalo mtu anakamatwa kwalo;
(a) Iwapo, kwa sababu za mazingira ambayo anakamatwa, mtu huyo anapaswa kujua kiini cha kosa ambalo anakamatwa kwalo; au
(b) Iwapo, kwa sababu ya vitendo vyake mtu anayekamatwa anasababisha kushindikana kuelezwa kosa analokamatwa nalo na mtu anaye mkamata.
Imeandikwa na Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿