SHERIA YA MIKATABA SURA YA 345 KIFUNGU CHA 11&12.
Kila mtu mwenye umri wa mtu mzima na mwenye akili timamu, ambaye hajazuiwa na sheria yoyote, ana uwezo wa kuingia mkataba.
Makubaliano yanayofanywa na mtu ambaye hajatangazwa kuwa na uwezo wa kufanya mkataba, hayo kisheria ni batili.
Katika kufanya mkataba, mtu anasemekana kuwa na akili timamu wakati wa kufanya mkataba ikiwa ana uwezo wa kuelewa na kutafakari maslahi yake katika mkataba husika.
Mtu ambaye mara nyingi anakua na matatizo ya akili, lakini muda mfupi anakuwa timamu, anaweza kufanya mkataba wakati anapokuwa na akili timamu.
Mtu ambaye mara nyingi anakuwa na akili timamu, lakini muda mfupi anakuwa na matatizo ya akili, hawezi kufanya mkataba muda anaokuwa na matatizo ya akili.
Imeandikwa na mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿