MAANA YA WOSIA.
Wosia ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonyesha nia yake jinsi gani angependa mali yake igawanywe baada ya kufa kwake.
Aina na sifa za wosia
Wosia unaweza kuwa wa namna mbili; wosia wa mdomo na wosia ulioandikwa (wa maandishi).
Wosia wa maandishi lazima
1.Uandikwe kwa kalamu ya wino na sio kalamu ya risasi (inayoweza kufutwa futwa).
2. Muusia awe na akili timamu.
3. Utaje tarehe ulipoandikwa.
4. Utaje kuwa muusia anayo akili timamu na anausia kwa hiari yake mwenyewe.
5. Ushuhudiwe na mashahidi wanaojua kusoma na kuandika angalau wawili (mmoja wa ukoo na mwingine mtu baki), kama muusia anajua kusoma na kuandika.
6. Ushuhudiwe na mashahidi wasiopungua wane (wawili wa ukoo na wawili watu baki), kama muusia hajui kusoma na kuandika.
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿