SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI SURA YA 20 KIFUNGU CHA 21.
Afisa polisi au mtu mwingine hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kutumia nguvu zaidi au kuvunja utu wa mtu huyo zaidi ya ilivyo lazima kufanikisha ukamataji au kumzuia utorokaji wa mtu baada ya kukamatwa.
Afisa polisi hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kufanya kitendo kinachoweza kusababisha kifo kwa mtu huyo, isipokuwa kama afisa polisi anaamini kwa sababu za msingi kwamba kufanya kitendo hicho ni muhimu katika kulinda maisha au kuzuia madhara makubwa kwa mtu mwingine.
Imeandikwa na Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿