Ticker

6/recent/ticker-posts

NI MARUFUKU MTOTO CHINI YA MIAKA 5 KUKAA SEAT ZA MBELE KWENYE GARI

 


SHERIA YA USALAMA BARABARANI KUPITIA MAREKEBISHO YA MWAKA 2016, KIFUNGU CHA 39D KILIONGEZWA.


Katika kifungu cha 39D(2) cha sheria ya usalama barabarani, mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 5 haruhusiwi kukaa siti za mbele katika gari akiwa peke yake au akiwa na MTU mzima, haruhusiwi kwa namna yoyote kukaa siti za mbele.


Lakini katika kifungu cha 39D(3), MTU hataruhusiwa kubeba mtoto katika gari binafsi, bila kuwa na vizuizi maalumu katika siti vyenye ukubwa na urefu unaomtosha mtoto kwaajili ya usalama wake.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )

Wa Jungu la sheria Tanzania

0758218269/0628729934

Chapisha Maoni

0 Maoni