Ticker

6/recent/ticker-posts

NDOA ILIYOVUNJIKA NA HAIREKEBISHIKI.



NDOA ILIYOVUNJIKA NA HAIREKEBISHIKI.

SHERIA YA NDOA ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2019, KIFUNGU CHA 171(2).

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa, ili ndoa ivunjwe na mahakama, ni lazima ushahidi utolewa unaoonyesha kwamba ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika.

Zifuatazo ni sababu zinazoonyesha kwamba ndoa imevunjika na haiwezi kurekebishika Tena.

(i) Kama mmoja wa wanandoa amemkimbia mwenziwe kwa muda usiopungua miaka mitatu na hajulikani alipo.

(ii) Ukatili.

-Kipigo;

-Malalamiko yasiyo na msingi;

-Mume anapolewa sana kila siku na kumbughuzi mkewe;

-Mume au mke anapomwambukiza mwenziwe maradhi ya zinaa.

(iii) Mmoja kati yao kufungwa maisha au kipindi kirefu kisichopungua miaka 5 au kuwekwa kizuizini.

(iv) Magonjwa ya uhanithi.

(v)Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile/kulawiti

(vi) Ugoni.

(vii) Uasi/utoro.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )

Wa Jungu la sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni