Sheria za hakimiliki zinalenga kulinda maslahi ya watungaji wa kazi za akili dhidi ya matumizi holela ya kazi zao na watu wengine bila kibali kutoka kwa mmiliki wa haki ya kunakili.
Kwa mujibu wa sheria za hakimiliki, kazi ya kiakili inaweza kunakiliwa pekee ikiwa mmiliki anatoa kibali cha kuruhusu kazi yake kunakiliwa. Ikiwa mtu ananakili kazi ya mtu mwingine bila kibali, anakiuka sheria za haki miliki, na inaweza kupelekea mashtaka ya madai au jinai juu yake kutegemeana na sheria za nchi husika.
Mkiukaji wa sheria za haki miliki anaweza kukumbana na hukumu ya kulipa fidia au hata kwenda jela anaposhindwa kulipa fidia. Kwa kawaida, sheria za hakimiliki hulinda haki za watungaji na warithi wao kwa kipindi fulani ambacho kinaweza kuongezwa endepo bado mmiliki wa haki miliki atahitaji kuongeza muda wa umiliki.
Imeandikwa na mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa @yesayajm_
Wa Jungu la sheria Tanzania.
0758218269/0628729934
0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿