Ticker

6/recent/ticker-posts

Aina za mahakama Tanzania.



Tanzania tuna aina 5 tu za mahakama katika mfumo wa utoaji HAKI wa kimahakama ambazo ni;


1. Mahakama za mwanzo.

2. Mahakama za wilaya.

3. Mahakama za mahakimu wakazi.

4. Mahakama kuu.

5. Mahakama ya rufaa.


Mahakama za mwanzo huanzishwa katika ngazi ya kila kata na husikiliza kesi za madai na zile za jinai zenye makosa madogo madogo ambayo adhabu yake haizidi mwaka mmoja jela.


Lakini upande wa madai, mahakama hizi husikiliza madai yenye thamani kati ya milioni 30 mpaka hamsini.


Mahakama kuu ina nguvu zaidi ya mahakama ya mwanzo.


#sherianatehama

#sheria

Chapisha Maoni

0 Maoni