Ticker

6/recent/ticker-posts

Ni KOSA LA JINAI KUPIGA PICHA MAITI



Ni KOSA LA JINAI KUPIGA PICHA MAITI. Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ni kosa la jinai kupiga picha au kusambaza picha zinazoonyesha maiti au miili ya watu waliofariki katika AJALI au wahanga wa tukio lolote ambao wamejeruhiwa vibaya. Adhabu ya kosa hili ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au adhabu ya faini isiyopungua milioni moja.


Haitakuwa KOSA endapo picha za maiti zimepigwa kwa lengo la kufanya uchunguzi wa kijinai, picha za nyakati za mazishi kwa lengo la kumbukumbu ya familia, au kama picha zimepigwa kwa kibali maalumu.


#sherianatehama 

#sheria

Chapisha Maoni

0 Maoni