Kushawishi Askari Kuacha Kazi Kosa la Jinai 🚫🪖👮🏽♂️
Kwa mujibu wa Kifungu cha 47 cha Kanuni ya Adhabu, kushawishi au kusaidia askari wa Polisi, Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa kuacha kazi bila ruhusa ni kosa la jinai.
🔹 Kosa hili linahusisha:
(a) Kushawishi au kujaribu kushawishi askari kuacha kazi.
(b) Kusaidia au kushiriki katika njama za kuondoka kwao.
(c) Kumficha au kumsaidia askari mtoro huku ukijua hali yake.
⚖️ Adhabu:
🔒 Kifungo cha miezi sita (6).
#JunguLaSheria 🇹🇿

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿