Ticker

6/recent/ticker-posts

Ndoa Inaweza Kubadilishwa Aina kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania.



Ndoa Inaweza Kubadilishwa Aina kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Sheria ya Ndoa, ndoa inayofungwa Tanzania inaweza kubadilishwa aina yake kama ifuatavyo:

🔄 Kutoka ndoa ya mke mmoja kwenda kwenye ndoa ya wake wengi.

🔄 Kutoka ndoa ya wake wengi kwenda kwenye ndoa ya mke mmoja— lakini mume awe na mke mmoja tu kwa wakati huo.

📜 Masharti ya mabadiliko haya:

Mabadiliko lazima yafanyike kwa tamko la maandishi linalotolewa kwa hiari na kwa pamoja na wanandoa wote wawili.

Tamko hilo lifanywe mbele ya jaji, hakimu mkazi au hakimu wa wilaya, lisainiwe na wahusika wote pamoja na hakimu au jaji na nakala kupelekwa kwa Msajili Mkuu wa Ndoa.

❌ Masharti mengineyo:

Ndoa ya Kikristo iliyofungwa kanisani haiwezi kubadilishwa kuwa ya wake wengi kwa muda wote ambao wanandoa wote wawili bado ni waumini wa dini ya Kikristo.

#SheriaYaNdoa #JunguLaSheria

Chapisha Maoni

0 Maoni