⏳ Muda wa Uhai wa Ndoa Kisheria.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 12 cha Sheria ya Ndoa, ndoa yoyote — iwe imefungwa Tanzania Bara au nje ya nchi — huendelea kuwepo kisheria hadi pale itakapovunjwa kwa moja ya njia zifuatazo:
⚰️ (a) Kwa kifo cha mmoja wa wanandoa;
📜 (b) Kwa amri ya mahakama inayotangaza kuwa mmoja wa wanandoa anahesabiwa kuwa amekufa;
❌ (c) Kwa amri ya kutengua ndoa;
💔 (d) Kwa amri ya talaka ya kisheria;
🌍 (e) Kwa talaka isiyopitia mahakamani iliyotolewa nje ya Tanzania lakini inakubalika na kutambuliwa kisheria hapa nchini.
#SheriaYaNdoa #JunguLaSheria

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿