⚖️ PORNOGRAFIA YA WATOTO MTANDAONI — NI KOSA KUBWA LA JINAI ⚖️
Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kimtandao [Sura ya 443 Toleo la 2023], Kifungu cha 13, ni kosa la jinai:
❌ Kuchapisha au kusambaza maudhui ya kingono yanayohusisha watoto kupitia mfumo wa kompyuta.
❌ Kuwezesha au kurahisisha upatikanaji wa maudhui hayo mtandaoni.
📌 Adhabu yake ni kali sana:
Faini isiyopungua Shilingi Milioni 50, au
Mara tatu ya faida iliyopatikana, Au kifungo kisichopungua miaka 7, au vyote kwa pamoja.
⚠️ Mahakama pia inaweza kuamuru fidia kwa mtu aliyeathirika na kosa hilo.

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿