📜 Unaweza kuweka pingamizi kuzuia kutolewa kwa usimamizi wa mirathi kwa mtu asiye na haki ya usimamizi.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uthibitishaji Wosia na Usimamizi wa Mirathi Sura 352, Kifungu cha 58:
• Mtu mwenye maslahi katika mali ya marehemu anaweza kuweka pingamizi dhidi ya maombi ya mtu mwingine anayeomba usimamizi wa mirathi.
• Pingamizi linaweza kuwekwa Mahakama Kuu au katika mahakama ambapo ombi la usimamizi limewasilishwa.
⚠️ Pingamizi huzuia utolewaji wa usimamizi wa mirathi mpaka hoja ya mleta pingamizi itakapochunguzwa na kutolewa maamuzi.
📚 Linda haki yako ya mirathi kwa kuchukua hatua sahihi za kisheria.
#JunguLaSheria ⚖️
#ElimuYaSheria 📚
#Mirathi

0 Maoni
WEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿