Ticker

6/recent/ticker-posts

Tafsiri ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika Sheria.Na Johnson Yesaya. LL.B.



Umewahi kusikia unyang'anyi wa kutumia silaha?

Hili ni kosa la unyang'anyi, wizi au ujambazi ambalo linafanywa kwa nguvu ya silaha.

Mtu anayeiba kwa kutumia silaha, au baadae ya kuiba analazimika kujilinda kwa silaha, Basi MTU huyo anakuwa ametenda kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Kosa hili limetajwa katika kifungu cha 287A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 TOLEO LA MWAKA 2019. Adhabu ya kosa hili ni kifungo cha miaka si chini ya 30 pamoja na au bila adhabu ya viboko.

Chapisha Maoni

0 Maoni