Kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyakazi hasa katika kampuni binafsi kufanya kazi bila mkataba, hii ni hatari sana na si salama kwa wafanyakazi hao.
Kufanya kazi bila Mkataba kuna hatari nyingi sana. Kwanza, kukosekana kwa ushahidi wa mfanyakazi kuwa ameajiriwa na mwajiri fulani kwa makubaliano halali, hivyo humuweka hatarini mfanyakazi huyo kupoteza haki zake za msingi linapokuja suala la migogoro Kati ya mwajiri na mwajiriwa hasa kufukuzwa kazi.
Mkataba wenyewe pia unahitaji vigezo kadha wa kadha kwa lengo la kukidhi matakwa ya kisheria ili mkataba huo uweze kumlinda mfanyakazi.
MAANA YA MKATABA
Mkataba wa Ajira ni Makubaliano yanayofanywa na Mtu au Taasisi inayoitwa Mwajiri kwa upande mmoja, na Mtu anayefahamika kama Mwajiriwa kwa upande mwingine kwa Lengo la kuainisha Haki na Wajibu wa pande hizi mbili.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, namba 6 ya 2004, Mwajiri ni Mtu au Taasisi inayomlipa Mtu mwingine Ujira kwa ajili ya kutoa Huduma, Ujuzi au Nguvu kazi inayofanikisha shughuli zake.
Mwajiriwa ni MTU mwenye ujuzi fulani ambaye ameajiriwa kwaajili ya kuwezesha kazi au uzalishaji katika shughuli ya mwajiri na kulipwa ujira au mshahara kama fidia ya kazi na ujuzi wake unaotumika.
AINA ZA MIKATABA
Aina ya Kwanza ya mikataba, ni mikataba ya kudumu.
Mikataba hii haiainishi ukomo wa Ajira na haielezi Ajira itachukua muda gani.
Aina ya Pili, ni Mikataba ya muda maalum unaofafanua ukomo wa Ajira husika.
Ukomo unaweza kuwa Mwezi mmoja, Mwaka mmoja, miwili, mitatu au vinginevyo. Kwa kutumia Mkataba huu, muda ulioelezwa kwenye Mkataba huo utakapokwisha, huo ndio unakuwa ukomo wa Ajira.
Tatu, ni Mkataba wa Jukumu/Shughuli maalum. Hapa Mwajiriwa anapewa Mkataba wa kukamilisha Kazi mahususi.
Kazi hiyo inapokamilika, huo ndio unakuwa ukomo wa Mkataba.
Kwa mfano, Mtu anaweza kupewa Mkataba wa kuandika Mradi. Kazi hiyo ya kuandika Mradi itakapokamilika, Mkataba huo unakuwa umefikia mwisho.
MAMBO MUHIMU KWENYE MKATABA
Bila kujali Mfumo wake, Mkataba hutaja upande unaotoa Kazi na upande unaokubali Kazi hiyo; kuitaja Kazi husika na kiwango Cha mshahara katika kazi hiyo.
Kutaja ukomo wa kazi kama upo, tarehe ambayo mkataba unaanza rasmi.

1 Maoni
Kwa mfano mtu kama fanya kazi miaka 6 na hakuwa na mkataba alafu akaachishwa kazi haki yake inalipwa vipi?
JibuFutaWEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿