Ticker

6/recent/ticker-posts

UNAJUA MAANA YA KINGA YA KIDIPLOMASIA? Na Johnson Yesaya. LL.B.



Basi tukufahamishe kuwa, kinga ya kidiplomasia ni kanuni ambayo inazuia kukamatwa, kuwekwa kizuizini au kufunguliwa mashtaka watu ambao ni wafanyakazi au wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, mabalozi, wafanyakazi wa balozi,  na familia zao.

Watu hawa hawapaswi kukamatwa na polisi wala kufunguliwa mashtaka katika mahakama za Taifa walilopo. Kinga hiyo inaweza kuondolewa na Taifa lililotuma maofisa hao wenye kazi ya kibalozi endapo inaonekana bayana kuwa maofisa hao wametenda makosa makubwa kabisa ambayo yanatishia usalama na amani ya Taifa walilofikia.

Kinga inapoondolewa wanaweza kukamatwa na kushtakiwa kama raia wa kawaida.

Chapisha Maoni

0 Maoni