Ninawezaje kupata nakala ya cheti cha ndoa iwapo cheti halisi kilipotea?
- Ndoa zote zinazofanyika Tanzania bara husajiliwa na kupata usajili wa msajili mkuu wa ndoa na talaka. Wasajili wote wa wilaya na viongozi wa dini wanatakiwa kisheria kutuma ndoa zote walizozifungisha kila mwishoni mwa mwezi. Kupitia katika taarifa hizi msajili mkuu kutunza kumbukumbu zote za ndoa.
- Iwapo cheti halisi kimepotea unaweza kupata nakala ya usajili ya ingizo la ndoa ambalo huhifadhiwa na msajili mkuu.Jinsi ya Kufanya ;
- Wasilisha maombi yako kwenye ofisi za RITA ukionyesha majina ya wanandoa, mahali ilipofungwa, wilaya pia onyesha iwapo ni ndoa ya kiserikali au ya kidini.
- Lipa ada halisi ambayo kwa sasa ni Tsh. 30000/= inayojumuisha yafuatayo:- TSH 10000/= ada ya utafutaji.- TSH 20000/= ada ya cheti.
2 Maoni
Rita imesaidia sana na pia imerahisisha huduma hongera sana.
JibuFutaNashauri kuandaliwe masomo yanayohusu sheria ya ndoa yawe yanafundishwa Shule za sekondari ilikujenga uelewa kwa jamii yetu ya kitanzania.
JibuFutaWEKA MAONI YAKO HAPA.
TAFADHALI USITUMIE LUGHA YA MATUSI AU KUUDHI KWANI NI KOSA KISHERIA.
KARIBU SANA NA ASANTEE.. 🇹🇿