Ticker

6/recent/ticker-posts

UHALIFU WA KIVITA NA MAKOSA DHIDI YA UBINADAMU.



Wakati huu wa vita vya RUSSIA na UKRAINE maneno ya "uhalifu wa kivita" na "makosa dhidi ya ubinadamu" yamekuwa yakitumika sana, je nini maana za makosa haya KISHERIA.


Kwa mujibu wa IBARA ya 8 ya "ROME STATUTE OF THE INTERNATIONAL CRIMINAL COURT", mkataba unaoanzisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai, uhalifu wa kivita ni vitendo vyote vinavyohusisha;


1. Mauaji ya raia wasio na hatia

2. Uharibifu wa mali za kijamii kama shule, hospitali, na maeneo ya ibada.

3. Kulazimisha mateka wa kivita kupigana dhidi ya majeshi yao ya asili.

4. Kusambaza silaha kinyume cha sheria.

5. Kujeruhi au kuumiza watu ambao wamelindwa na maktaba wa Geneva.


MAKOSA DHIDI YA UBINADAMU.


Kwa mujibu wa IBARA YA 7 ya mkataba tajwa hapo juu, makosa dhidi ya ubinadamu ni makosa yote yanayofanywa dhidi ya au kwa kulenga kwa makusudi kikundi fulani cha watu katika jamii.


Makosa yanayolenga kikundi fulani cha watu yanaweza kuwa ni kuua, kulemaza au kujeruhi, kufunga gerezani, au kuwahamisha kwa nguvu watu wa kundi fulani (kabila, dini, au rangi za ngozi) kwenda sehemu nyingine bila ridhaa yao.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa @yesayajm_

Wa Jungu la sheria Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni