Ticker

6/recent/ticker-posts

UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUBADILI JINA KABISA.



UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUBADILI JINA KABISA.


Ni kweli inawezakana kubadili jina kabisa au kurekebisha sehemu ya majina yako kupitia "KIAPO".


Kiapo cha kubadili jina ni nyaraka ambayo inaweza kuandaliwa na wakili au mahakama, ambapo nyaraka hiyo inakuwa na majina ya awali na majina mapya ambayo muapaji anayahitaji.


Baada ya kiapo hicho kukamilika kadri inavyotakiwa kisheria basi majina ya muapaji yatakuwa yamebadilika na muapaji atatumia kiapo hicho kubadilishia majina yake katika nyaraka zingine kama vyeti vya masomo, hati za umiliki ardhi n.k

Chapisha Maoni

0 Maoni